Technology

Fahamu video ya wimbo mpya wa ‘A Good Night’ wa John Legend imeshutiwa kwa simu

Zikiwa zimepita siku nne tangu msanii wa muziki wa R’n’B kutoka Marekani, John Legend kuachia video ya wimbo wake mpya wa ‘A Good Night’. Hatimaye mkali huyo wa R’n’B amefunguka kuwa video ya wimbo huo imeshutiwa kwa kutumia simu aina ya Google Pixel 2.

Tokeo la picha la A Good Night john legend shot by pixel 2
Picha za Behind the Scene wakati wa uaandaaji wa video hiyo.

John Legend amethibitisha taarifa hizo kwenye mahojiano yake na mtandao wa Google amesema sababu kubwa ya kufanya hivyo amesema anaamini kuwa Google Pixel 2 ni simu yenye kamera bora zaidi kuliko smartphone yoyote duniani, ingawaje amekiri wazi kuwa alipatwa na hofu kushuti kwa kutumia simu kwani video hiyo imetumia bajeti kubwa kuiandaa.

Tokeo la picha la john legend a good night taken by google pixel 2

John Legend ameongeza kuwa alipata wazo hilo la kutumia simu kutokana na maudhui ya wimbo wake ambao unaelezea mwanaume/mwanamke aliye-single anayetafuta mwenza kupitia kwenye mitandao ya kijamii na wanakutana kwenye klabu wanamaliza haja zao na kuachana usiku huo huo.

Nilipata wazo la kutumia simu janja (Smartphone) google Pixel 2 kusema kweli ni moja ya simu zenye kamera za ajabu duniani, na ilinipa tabu sana kipindi tunawasilisha wazo hilo kwa waongozaji wangu kwani nilitoa fedha nyingi sana kuandaa video hii. Lakini nashukuru Mungu wimbo umeenda kama nilivyokuwa nataka yaani rangi na muonekano wa klabu ni moja ya vitu vilivyonogeshwa kwenye video.“amesema John Legend.

John Legend amesema video ya wimbo huo yote imeshutiwa na simu hizo janja na tayari video hiyo imeshatazamwa mara milioni 1.3 kwenye mtandao wa Youtube.

Tokeo la picha la john legend a good night taken by google pixel 2

Toleo la simu aina ya Google Pixel 2 ni moja ya matoleo bora ya simu za Google ukiacha toleo jipya la simu hizo aina ya Google Pixel 2 XL.

Google Pixel 2

Baadhi ya sifa za Pixel 2 ni kwamba ina kamera yenye ukubwa wa Megapixel 12 pekee na flash mbili ambazo zinasaidia kutoa picha nzuri na zenye ubora. Na simu hizo zinaukubwa wa ndani GB 64/128 na hazina sehemu ya kuweka Memory Card.

Tazama video hiyo ya ‘A Godd Night’ hapa chini ambayo John Legend amemshirikisha BloodPop;

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents