Habari

Familia ya kifalme ya Uingereza yapata mtoto wa kike

Kate Middleton (The Duchess of Cambridge) amejifungua mtoto wa kike, kwa mujibu wa ikulu ya Kensington ya nchini Uingereza.

0780A07C00000514-3044227-Growing_family_Prince_William_was_with_33_year_old_Kate_througho-a-184_1429307197569

Mtoto huyo amezaliwa salama leo asubuhi saa 2:32. Prince William (The Duke of Cambridge) alikuwepo wakati mtoto huyo anazaliwa akiwa na uzito wa (3.7kg).

Mama na mwana wote wanaendelea vyema kwa mujibu wa maelezo hayo.

Jina la mtoto huyo litatangazwa baadaye. Watu wengi wamekusanyika kwenye hospitali ya St Mary’s kufurahia ujio wa mtoto huyo.

Wawili hao wana mtoto mwingine, Prince George of Cambridge

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents