Burudani

Fid Q kuachia video ya ‘Walk it Off’ wikiendi hii

Fareed Kubanda aka Fid Q anatarajia kuvunja ukimya kwa kuachia video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Walk it Off’ aliomshirikisha Taz.

12558347_852177044904109_571092224_n
Fid Q akitengenezwa vyema nywele zake kabla ya kushoot video hiyo mwishoni mwa mwaka jana

Video ya wimbo huo ilifanyika nchini Afrika Kusini mwishoni mwa mwaka jana. Imeongozwa na Nicroux wa kampuni ya Molotov Cocktail ya Afrika Kusini ambayo miongoni mwa video ilizofanya ni pamoja na Jealousy ya AKA na Rands and Nairas ya Emmy G.

Kupitia Instagram, Fid ameandika: #TANGAZO New visuals by FID Q @therealfidq feat TAZ – directed by @nicroux coming your way this weekend.. Stay tuned.”

Hiyo inakuwa video ya kwanza ya Fid Q kufanya Afrika Kusini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents