Burudani

Floyd Mayweather na 50 Cent wadaiwa kuzichapa kavu kavu


Bondia Floyd Mayweather amezinogesha fununu kuwa alizichapa kwa mara nyingine tena na swahiba wake 50 Cent, kwa kuandika kwenye Twitter kuwa watakuwa na “round two.”

Bingwa huyo wa welterweight aliyemshinda Miguel Cotto mwezi huu, anasemekana kuzichapa na rapper huyo katika weekend ya siku ya kumbukumbu nchini Marekani.

Inasemekana kuwa sababu ya ugomvi huo ni kutokana na 50 kudaiwa $10,000 na Floyd.

Japokuwa hawakuthibitisha stori hizo, Floyd alipost picha inayomwonesha akiwa amekunjiana ngumi na Fifty huku mtu mmoja akiwa katikati yao na pesa mkononi.

“Round 2: Me and @50Cent getting it on over some stacks..,” Floyd aliandika maelezo hayo kwenye picha hiyo.

Hata hivyo inaonekana kama maswahiba hawa wanatafuta tu kitu cha kuzungumziwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents