Habari

Fly-SAX: Shirika la ndege linalotarajia kuanza safari Tanzania, litakuwa mshindani mkuu wa Fastjet

Shirika la ndege la Kenya, Fly-SAX huenda likaanza safari zake nchini Tanzania ambapo sasa linasubiri tu kupewa ruhusa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini. Shirika hilo linalofahamika kwa gharama zake ndogo litakuwa mshindani mkuu wa fastjet PLC.

2143853

SAX-Tanzania inatarajia kuanza safari kwenye nusu ya pili ya mwaka huu kwa ndege zake ndogo zinaZOchukua abiria 12 hadi 80 na pia itakuwa ikifanya safari za mikoani zaidi. Pia Fly-SAX ina matarajio ya kupewa kibali cha kuwa na ndege za kimataifa kutoka Tanzania.

“Tunaanzisha kampuni mpya ya ndege kukidhi mahitaji ya ndege za gharama ndogo, salama na za uhakika ndani ya Tanzania kwaajili ya wananchi wake na watalii wa kitaifa,” alisema CEO wa Fly-SAX na Fly 540 Kenya Don Smith.

Fly-SAX imeshamteua Brown Francis kama Mkurugenzi Mkuu wa SAX-Tanzania. Francis anatokea fastjet, ambako alikuwa mkurugenzi industry affairs kwa Tanzania.

Chanzo: The Wall Stree Journal

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents