Burudani

G-Nako asema anatamani video yake mpya ifike level za kimataifa lakini kuna changamoto

G-Nako kutoka Weusi amesema kuwa anatamani video yake mpya ‘Sichezi Mbali’ aliyofanya na director mchanga wa Arusha (Cyne Studios) ifike kwenye vituo vya kimataifa kama MTV na Trace , lakini kuna changamoto zinazofanya kuwe na ugumu.

“Hiyo level kila mtu anataka kuifikia, lakini kuna changamoto zake pia, utaona kwa mfano mimi nimetoa video yangu mpya lakini nimefanya na director mchanga kabisa kutoka Arusha, na ni video ambayo ni kali.” Alisema G-Nako.

Akizungumza kupitia kipindi cha Genge cha E-FM, Warawara amesema kuwa video inapofanywa na director wa nje inakuwa na uhakika wa kuoneshwa na vituo hivyo kutokana na waongozaji hao wa nje kuwa na connection na vituo hivyo.

“Lakini linapokuja swala la video zetu kwenda kuchezwa kwenye channel zingine, ma-directors pia wa nje wanakuwa na channels zao, kwasababu wanakuwa na ukaribu zaidi na vituo vya televisheni ambavyo vipo pale na connection inakuwa rahisi zaidi. Lakini naamini kuna kazi ambazo zimeshafanyika ambazo pia zinaweza zikaenda katika level hizo, isipokuwa tu namna ya kuzifikisha na channel ambazo tunazo.”

joh mtv

Video ya wimbo wa Joh Makini ‘Nusu Nusu’ ambayo G-Nako pia ameshiriki kwenye wimbo na kuonekana kwenye video hiyo ambayo imefanywa Afrika Kusini na Justin Campos, wiki hii imekamata nafasi ya sita kwenye Official African Chart ya MTV Base.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents