Habari

Gondwe awataka wazazi kuacha kuwaficha watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Handeni, anaye kaimu Ukuu wa Mkoa wa Tanga kwa sasa, Mh Godwin Gondwe alipotembelea kambi tiba ya GSM Foundation yenye lengo la kuokoa watoto zaikai ya 3500 wanaodaiwa kupotea maisha kila mwaka kutokana na kuzaliwa na tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi.
6g

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe akigawa fedha za nauli kwa mmoja kati ya wakazi wa wilaya hiyo Mwajuma Rashid ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mkaramo wilayani Handeni mara baada ya kufika kwenye hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo.

Gondwe aliipongeza taasisi inayojihusisha kusaidia sekta ya Afya na Elimu hapa nchini kwa kutoa matibabu ya upasuaji huo kwa watoto hali ambayo itawasaidia kuweza kurejea kwenye hali zao za kawaida.

Alisema katika suala kama hilo jamii haina budi kuacha kuwaficha watoto wenye matatizo hayo badala yake waona namna ya kuwasiliana na viongozi wao ngazi za chini kuwaepusha na vifo ambavyo vinaweza kuwakumba kutokana na hali walizonazo.

“Lakini pia lazima jamii ibadilike kuona umuhimu wa kuacha kuwaficha watoto wenye matatizo hayo badala yake wawapeleke kwenye hospitali zilizopo karibu nao kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambayo yatawasaidia kupona “Alisema.

Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakazi wa zoezi la Upasuaji wa watoto hao lilipokuwa likiendeshwa na madaktari Bingwa, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji ya (MOI)iliyopo Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili, Dkt Othman Kiloloma alisema ongezeko la watoto hao linatokana na ukosefu wa lishe yenye virutubisho vijulikanavyo kwa jina la “Folic Acid”

Alisema kukosekana kwa lishe hiyo kumesababisha tatizo hilo kwa watoto ambalo lisipopatiwa ufumbuzi wa kina linaweza kupelekea athari kubwa kwao ikiwemo vifo hali inayoweza kupunguza jamii ambayo ingeweza kuchangia ukuaji wa uchumi katika shughuli za uzalishaji.

“Ukiangalia kwa hivi sasa zaidi ya watoto wapato 4000 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi huzaliwa kila mwaka nchini na wanaoripotiwa hospitalini si zaidi ya 500 hatua ambayo imechangia kwa asilimia kubwa ongezeko la watoto wenye mtindio wa ubongo huku baadhi yao wakipoteza maisha kwa sababu ya kukosa hivyo jamii inapaswa inapaswa kuwapeleka katika Hospitali ili kuweza kuchangia ukuaji wao na maendeleo “Alisema

Kwa upande wa Afisa Habari wa Taasisi ya Afya inayojihusisha na Upasuaji wa watoto hao, Khalfani Kiwamba alisema kuwa upungufu wa madaktari wenye taaluma ya upasuaji wa waathirika hao ni mkubwa kwa sababu nchini wapo saba ambapo sita wapo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na mmoja yupo hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Bugando

Kufuatia hatua hito, Viongozi wa Taasisi za dini nchini zimeshauriwa kuwahamasisha waumini wao wenye watoto wa aina hiyo kuwafikisha katika Hospitali kubwa za Rufaa ili waweze kushauriwa badala ya kuwaficha watoto hao majumbani ambapo wanapofikisha miaka kumi na kuendelea uwezekano wa kupoteza maisha ni mkubwa sana.

“Kwani hatua hiyo imechangia kwa asilimia kubwa ongezeko la watoto wenye mtindio wa ubongo huku baadhi yao wakipoteza maisha kwa sababu ya kukosa tiba “Alisema

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents