Michezo

Guardiola: Yaya Toure lazima aombe msamaha la sivyo hatocheza tena

Kochaa wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amefunguka kuwa hatomchezesha tena Yaya Toure hadi atakapoomba msamaha kwa klabu hiyo na wachezaji wenzake kutokana na matamshi ya ajenti wake.

_91316222_guradiolanyayatoure

Toure mwenye umri wa miaka 33 ameichezea City mara moja msimu huu na aliwachwa nje katika kikosi cha vilabu bingwa Ulaya.
Ajenti wake Dimitri Seluk amesema kuwa kiungo huyo wa kati ”alifedheheshwa” na kwamba Gurdiola anafaa kumuomba msamaha iwapo City haitashinda kinyang’anyiro hicho.

Guardiola:”lazima aombe msamaha la sivyo hatocheza”.
Raia huyo wa Uhispania pia anataka msamaha kutoka kwa Seluk.

Alisema kuwa ni uamuzi mgumu kumwacha nje Toure katika kikosi cha kombe la Vilabu bingwa Ulaya.
”Iwapo ana tatizo anafaa kuzungumza wenzake katika klabu ,alisema Gurdiola,ambaye alikuwa mkufunzi wa Barcelona wakati Toure alipouzwa kwa Manchester City 2010.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents