Michezo

Grand Rapids Drive: Tutamrudisha Hasheem Thabeet NBA

Timu ya Grand Rapids Drive inayocheza kwenye NBA-D League inaamini kuwa Hasheem Thabeet hakupewa muda wa kutosha kucheza kwenye timu alizokuwa akichezea NBA na ndio maana performance yake ilikuwa hairidhishi.

-aa75c72ee6f78afe

Katika misimu yote mitano aliyocheza na timu nne, alikuwa na wastani wa pointi 2.2, rebounds 2.7 na blocks 0.8 katika kila mchezo. Kocha wa Grand Rapids Drive Otis Smith, amesema ana mpango wa kumpa nafasi Thabeet kuonesha kipaji chake akiwa na timu hiyo.

“Ningependa kuamsha career yake. Hicho ndicho nilichomuambia,” alisema Smith said. Ni kama msuli ambao haukuwa ukifanya kazi vyema. Unahitajika kufanya vitu tofauti kumsha hilo. Ningependa kumpa nafasi zaidi, kumpa dakika nyingi ili ajisikie comfortable kucheza kwa muda mwingi. Hakuwa na nafasi kabisa kwenye NBA na kupewa muda mwingi wa kucheza. Lakini tunaenda kubadilisha vitu ili kumfanya awe comfortable na hilo.”

Katika miaka ya 2008-09, Thabeet alijinyakulia sifa kwa uwezo wake wa kuzuia magoli wakati akicheza chuoni. Alikuwa na wastani wa pointi 13.6, 10.8 rebounds na blocks 152. Alitajwa PIA kama mlinzi bora wa mwaka.

“Wengi wetu huja kutoka tutokako na kuwa na mtazamo na ligi kwamba utaenda kucheza kama ulivyofanya chuoni,” anasema Thabeet. “Mambo hayaendi hivyo. Unatakiwa kujifahamu. Na hii ni fursa ya kujifahamu na kufanya kile nifanyacho kwa ubora – kuzuia mipira ya kucheza safu ya ulinzi.

Thabeet alizitupitia mbali ofa za kucheza ulaya na kuamua kuchukua mkataba wa D-League.

“Nimepata ofa chache na watu kadhaa walinitafuta,” alisema. Labda, lakini hapana, kwa sasa mimi nataka kucheza na nina nafasi hiyo hapa.”

Tatizo lake kubwa lilikuwa ni faulo. Thabeet alikuwa akipata faulo moja kila dakika tano.

Kama mambo yakienda vizuri, Thabeet atachukuliwa tena na timu ya NBA. Na Smith anaamini mambo yataenda vizuri.

Chanzo: http://www.mlive.com

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents