Promotion

Una kipaji cha kuimba? Airtel Trace Music Stars inaweza kubadilisha maisha yako!

Kuna vipaji vingi vya muziki hapa nchini ambavyo kutokana na sababu mbalimbali, vimeshindwa kuonekana. Kikwazo kikubwa ni gharama za kuingia studio na kurekodi wimbo wenye kiwango kizuri cha kuchezwa redioni.

925551_1535936979984787_887222267_n

Hata kwa wale waliofanikiwa kurekodi nyimbo zao, bado wanakutana na vikwazo vingi pale wanapopeleka nyimbo zao kwenye vituo vya redio. Kutokana na kuwepo wingi wa nyimbo zinazopokelewa na vituo hivyo, ni wachache wanaopata bahati hata tu kusikia wimbo wao ukichezwa mara moja.

Lakini kuna tumaini kutoka Airtel na kituo cha Trace TV ambao wameshirikiana kuanzisha shindano la Airtel Trace Music Stars. Unachotakiwa ni kupiga simu kwenye namba 0901002233, imba wimbo wako na unaweza kuwa mshindi.

Hivyo hii ni habari njema kwa waimbaji, rappers na wengine wanaotafuta nafasi ya kutoboa kimuziki, kutengeneza fedha nyingi na kuwa mastaa. Shindano hili ni la kwanza kuhusisha simu tu kushiriki. Ni shindano la kwanza la uimbaji ambapo washiriki wanachotakiwa ni kupiga simu na kuimba nyimbo zao.

Hakuna haja ya kusimama kwenye mistari mirefu kama mashindano mengine ya aina hii yalivyo, simu yako ndio studio yako. Unachotakiwa kufanya ni kupiga, kuimba na kuwa na nafasi ya kuwa msanii mkubwa ajaye hapa nchini na barani Afrika kwa ujumla.

Piga sasa 0901002233, imba na ushinde.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents