Michezo
Gwiji wa soka, Pele afanyiwa upasuaji
Mfalme wa soka duniani, Pele amefanyiwa upasuaji ili kuondoa uvimbe kwenye koloni yake.
Pele mwenye umri wa miaka 80, alikuwa amelazwa hospitalini kwa siku sita, siku ya Jumatatu aliandika kwenye mitandao yake ya kijamii akisema alifanyiwa upasuaji ili kuondoa ” Uvimbe unaoshukiwa kuwa kidonda,” Jumamosi iliyopita.
“Kwa bahati nzuri, nimezoea kusherehekea ushindi mkubwa pamoja nanyi,” alisema mshindi huyo mara tatu wa Kombe la Dunia.
Siku tano zilizopita, Mbrazil alikanusha ripoti kwamba alikuwa amezimia. Afya yake imekuwa ya wasiwasi katika miaka ya hivi karibuni.
Kulingana Guinness Book of World Records, alifunga mabao 1,279 yaliyoripotiwa katika mechi 1,363, pamoja na mabao 77 katika mechi 91 za kimataifa akiwa na Brazil.