Habari

Habida aja na ‘Girls Night Out’

Baada ya kuwa kimya tangu atoe Reason aliyomshirikisha Cannibal, mwanadada Habida kutoka Kenya sasa amekuja na single mpya iitwayo “Girls Night Out” aka GNO!

Na tayari wimbo huo umefanywa rekodi ya wiki na Homeboyz Radio ya Kenya.

Wakati video ya wimbo huo ikiwa inasubiriwa kwa hamu, Habida ametoa baadhi ya picha zilizochukuliwa wakati wa shooting ya video yake.

Katika wimbo huu uliotengenezwa na producer Silverstone Habida kabadilika kidogo. Unaweza kumfananisha na mnigeria lakini ukisikia maneno ya Kiswahili basi jibu utakuwa nalo kuwa ni mkenya.

Ni wimbo wa kucheza zaidi kuliko kusikiliza. Na kama ujumbe wake ulivyo, ni muda wa kinadada kutoka na kula bata bila hisani ya kidume chochote. Paying their own bills!

Usiku wa jana kupitia Twitter ameandika, “Back to the good stuff my new track Girls Night Out, GNO is now out and video coming soon! Now that’s good news for your ears!”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents