Burudani

Hanscana na Nisher waliwahi kushutumiana kuigana ideas wakati wote waliniiga mimi – Adam Juma

Hivi karibuni Adam Juma amekuwa akiendelea kutoa ‘makavu live’ kwa kile anachokielezea kama kukosewa heshima na vijana aliowatangulia kwenye fani ya uongazaji video za muziki.

11264234_422545727907055_1376403793_n

Muongozaji huyo mkongwe ameiambia 255 ya XXL, Clouds FM jana kuwa pamoja na watu wengi kudhani alipanic kwa kuandika post hizo, bado ujumbe huo uliwafikia walengwa.

Hata hivyo alisema kuwa hivi karibuni Nisher alimshutumu Hanscana kuiga idea yake ya video ya ‘XO’ ya Joh Makini na kuitumia kwenye video Jux, ‘Nikuite Nani’ bila kujua kuwa wote walimuiga yeye.

“Mtu akikopi kitu changu mimi ninakijua,” alisema Adam. “Walikuwa wanalaumiana kwamba huyu kamkopi huyu wakati wao wenyewe wamenikopi mimi, wenyewe hao madogo, mimi nimekausha, nimeuchuna tu. Wote yaani kuna kazi nikianza kuzipigia mstari, huyu kamkopi huyu, huyu kamkopi huyu na mwisho wake kanikopi mimi.”

Pamoja na hivyo, Adam amesema anajivunia kazi wanazofanya waongozaji hao na kwamba wanaiwakilisha vyema Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents