Burudani

Hanscana: Nipe bajeti nzuri mimi nitakufanyia video yenye International standards

Director wa video za muziki nchini, Hanscana amesema kuwa endapo wasanii watampa bajeti nzuri anauwezo wa kuwafanyia video nzuri na zenye viwango vya kimataifa.

hanscana4

Hanscana ametumia mfano wa video ya Belle 9 ‘Shauri Zao’ iliyoanza kuoneshwa Trace Tv jana, ambayo ameiongoza yeye na kushoot hapa hapa Tanzania.

Kupitia Instagram Hanscana ameandika;

“Imeshutiwa hapa hapa tz na director wa hapa hapa tz .

Nakuahudi Mteja wangu We nipe Bajeti nzuri sana me ntakufanyia video nzuuri sana na yenye International standards Na tutashirikiana bega kwa bega kuhakikisha inafika inapostahili kwa manufaa yetu sote na taifa kwa ujumla”

Katika mahojiano na Bongo5, Belle 9 aliwahi kusema video hiyo imegharimu shilingi milioni 12, na ndio video yake ya kwanza kutumia pesa nyingi kiasi hicho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents