Habari

Hashim Rungwe ana siku nne anashikiliwa na Jeshi la Polisi

Aliyekuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Hashim Rungwe Spunda anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa siku nne sasa.

Rungwe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chaumma) anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam akituhumiwa kughushi nyaraka.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema leo Septemba 5 kuwa, Rungwe anashikiliwa kituoni hapo kwa siku nne.

Hata hivyo, Kamanda Mambosasa hakutaka kuingia kwa undani kuhusu suala hilo akisema hana taarifa za kutosha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents