Burudani

Hata kama mimi ni DJ siwezi kupiga huo wimbo – Amini (+video)

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Amini amesema haamini kama kuna wasanii wanapendelewa kwenye media kwa kupewa airtime zaidi bali inategea na wakati husika.

Mumbaji huyo amesema kuwa licha ya wakati pia muziki mzuri au kazi nzuri ndizo zinapewa zaidi nafasi na si vinginevyo.

“Tusizungumzie airtime fulani anapendelewa, hapana!, Watanzania wanapenda kitu kizuri kwa sababu hata anayepiga muziki redioni au kwenye TV naye anapenda kitu kizuri,” Amini ameiambia Bongo5.

“Kwa hiyo kuna promotion na kitu kizuri, so lazima tufanye kitu kizuri ili tuweze kupata airtime. Hawezi kupiga wimbo mbaya, wewe uimbe nje ya biti au key, hata kama mimi ni DJ siwezi kupiga au presenter siwezi kuuzungumzia huo wimbo,” amesema.

Katika hatua nyingine Amini amesema kuwa hajaondoka THT bali kuna watu walimuhitaji afanye nao kazi kwa kipindi cha miezi sita na baada ya hapo amerudi THT kwa sababu ndipo nyumbani kwake kimuziki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents