Habari

Hatma ya Sabaya ya miaka 30 jela na wenzake wawili kujulikana leo

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, inatarajiwa kutoa hukumu ya rufaa ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, na wenzake wawili waliyoikata ili kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 kila mmoja iliyotolewa Oktoba 2021.

Hukumu ya rufaa hiyo inatarajiwa kutolewa hii leo Mei 6, 2022, dhidi Sabaya na wenzake Sylivester Nyegu na Daniel Mbura, baada ya hukumu iliyotolewa mwaka jana katika mahakama hiyo kuwakuta na makosa matatu ikiwemo la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents