Siasa

Hii ndio Safu mpya ya Sekretarieti Kuu ya CCM (+ Video)

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amempendekeza Daniel Godfrey Chongolo kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.

Chongolo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam, endapo ataidhinishwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho, atarithi mikoba ya Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ambaye ni mbunge.

Aidha, Mhe. Samia amempendekeza Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamidu Shaka kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa chama hicho kuchukua nafasi ya Humphrey Polepole ambaye aliteuliwa kuwa mbunge.

Safu mpya ya Sekretarieti Kuu ya CCM

Katibu Mkuu wa CCM- Ndg Daniel Chongolo (Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni)

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM- Ndg Shaka Hamdu Shaka (Anachukua nafasi ya Humphrey Polepole
ambaye ni Mbunge)

Katibu wa Uchumi na Fedha Frank George Hawasi aendelee na nafasi yake

Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa

Ngebela Lubinga aendelee na nafasi yake

Katibu wa NEC Oganaizesheni -Ndg Mama Maurdin Kastiko

Ndg Pereira Silima atapangiwa majukumu mengine ya kitaifa)

Naibu Katibu Mkuu Bara-Christina Mndeme (Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma) ndugu Rodrick Mpogolo atapangiwa majukumu mengine ya kitaifa)

Naibu Katibu Mkuu Zanzibar- Abdallah Juma Sadala Mabodi anaendelea na nafasi yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents