Michezo

Hizi ndio rekodi za Mesut Ozil kabla ya kutangaza kustaafu timu ya taifa

Hizi ndio rekodi za Mesut Ozil kabla ya kutangaza kustaafu timu ya taifa

Mchezaji wa klabu ya Arsenal na taifa la Ujerumani Mesut Ozil jana tarehe 22/7/208 ametangaza rasmi kujiuzulu kuitumikia timu yake ya taifa ya Ujerumani.

Ozil ametoa tamko hilo kupitia barua ambayo aliisambaza kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii,tamko hilo la Ozil limesisitiza zaidi suala la ubaguzi wa rangi ambavyo amedai amefanyiwa na baadhi ya viongozi wa shirikisho la mpira nchini Ujerumani (DFB) kutokana na asili yake kuwa ni asili ya Uturuki.

Huenda maneno yote haya ya kubaguliwa yalianza kujitokeza baada ya hapo kipindi cha nyuma Ozil kuonekana amepiga picha na mmoja wa viongozi a taifa la Uturuki na hapo ndipo suala la Ozil kuitwa msaliti na baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini Ujerumani lilipoibuka.

Kabla ya Ozil kutangaza kustaafu kulitumikia taifa hilo la Ujerumani alimaarufu German Mashine ameweza kuichezea Ujerumani katika mashindano mbalimbali.

Zifuatazo ni baadhi ya rekodi zake katika timu ya taifa ya Ujerumani,Ozil amefanikiwa kuitumikia timu hiyo michezo 92 akiifungia magoli 23 akitoa assists 33 pia akishinda tuzo ya mchezaji bora wa Ujerumani kwa nyakati 5 tofauti kuanzia mwaka 2011,2012,2013,2015 na mwaka 2016 huku akiisaidia timu hiyo kushinda taji la kombe la Dunia mwaka 2014 michuano iliyofayika nchini Brazil.

Mesut Ozil alizaliwa miaka 29 iliyopita Oct 15 mwaka 1988,alianza kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani chini ya miaka 19 mwaka 2006/07 chini ya miaka 21 mwaka 2007/09 na hatimaye kuanza kitumikia timu ya Ujerumani senior mwaka 2009 hadi July 22 mwaka 2018 alipotangaza kustaafu.

By Ally Jei.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents