Habari

‘Holela Holea Itakukosti’ yaendelea kuchanja mbuga

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanyia mazungumzo na KIDO ambaye ni balozi wa kampeni ya Holela-Holela itakukosti. Kampeni ya Holela-Holela itakukosti inasisitiza mbinu kamilifu ya ” Afya Moja” kushughulikia tatizo la UVIDA na magonjwa ya zuonotiki na ilizinduliwa Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi uliopita kwa uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana Wizara ya Afya, Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Wizara ya Mazingira huku ikifadhaliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kupitia mradi wa Breakthrough ACTION.

Akizungumza leo Jijini Dodoma baada ya kufanyia mazungumzo na balozi KIDO, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alisisitiza juu ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa (UVIDA) na magonjwa ya kipaumbele ya zuonotiki (magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu) ambayo kampeini ya Holela-Holela Itakukosti imelenga. ‘Naomba nichukue fursa hii nitoe wito kwa jamii kuwa Mtanzania anaweza kufanya mambo machache tu kukabiliana na UVIDA, kama vile kupata na kufuata ushauri wa mtaalamu wa afya kabla ya kutumia dawa, kutumia dozi ya dawa kikamilifu kama unavyoshauriwa na mtaalam wa afya, kufuata maelekezo ya mtaalam wa mifugo/kilimo juu ya matumizi sahihi ya dawa kwa mifugo/mimea, na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na usafi wa mazingiria kwa ujumla’.

Waziri Ummy aliongeza, ‘Suala la UVIDA ni tatizo kubwa sana, na athari zake ni kama vile ugonjwa kujirudia rudia na kuchukua muda mrefu kupona, kuenea na kusambaa kwa vimelea sugu vya magonjwa dhidi ya dawa, ulemavu na hata kifo. Mbali na hapo kuna athari za kiuchumi kama vile kutumia gharama kubwa kwenye matibabu, hivyo kupungua kwa pato binafsi, la familia na taifa’.
Waziri Ummy alisema kuwa Serikali inafanya jitihada kabambe za kukabiliana na UVIDA, ikiwemo kuzindua kampeni ya “Holela Holela itakukosti”, inayolenga kuongeza uelewa juu ya UVIDA na kuleta mabadiliko chanya ya tabia ili kukabiliana na UVIDA katika jamii.

Pamoja na kampeni hiyo upo mpango kazi wa mapambano ya UVIDA (NAP AMR 2023-2028), na kamati ya Taifa ya Mapambano ya UVIDA (AMR MCC) inayofanya kazi chini ya mwamvuli wa Afya moja. Vilevile kuna miongozo mbalimbali ya Kisekta inayosaidia katika mapamabano ya UVIDA”

Kwa Upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa USAID nchini Tanzania Alex Klaits alisisitiza umuhimu wa juhudi za pamoja, akisema, “Kampeni inaonyesha jukumu muhimu la ushirikiano katika kuleta athari chanya na kuhakikisha uendelevu wa muda mrefu, ikiwaleta pamoja wadau wa Afya moja kutoka sekta mbalimbali kupambana na UVIDA na magonjwa ya zuonotiki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents