Burudani

Homa Homa kumvuta RayVanny Congo?

Msanii wa muziki kutoka nchini Congo ambaye makazi yake ni nchini Ubeligiji, Homa Homa ambaye amekuwa akifanya muziki kwa miaka kadhaa, ameakuja kivingine na kuhaidi kuwa amejipanga kwa kiasi kikubwa kuhakikisha muziki wake unafika mbali zaidi.

Msanii huyo ambaye anaufuatilia muziki wa Tanzania amefunguka mengi kuhusu project mpya na maisha ya muziki.

Swali: Ni nini kilikuhimiza kuja na mfululizo wa ngoma ambazo umeziita Afro Bx?

Jibu: Wakati fulani katika kazi yangu niligundua haraka tofauti ambayo ni sifa yangu. Mimi ni kijana niliyekulia Congo na kwa sasa ninaishi Ubelgiji. Mchanganyiko huu wa kitamaduni huathiri muziki wangu moja kwa moja. Kwa kuwa na aina kuu, afrobeat, nilielewa haraka kuwa afro yangu itakuwa mchanganyiko wa athari kutoka kwa tamaduni hizi zote. Afro BX imetengenezwa kwa afro huko ubeligiji. Mchanganyiko wa utamaduni wangu wa asili na ule wa mazingira yangu mapya. Kwa ufupi, Afrobeat yenye miondoko ya muziki wa mijini unaozungumza lugha ya Kifaransa.


Swali: Ukipata nafasi ya kufanya kazi na msanii yeyote wa Tanzania ambaye yupo kwenye mawazo yako kwa sasa na kwanini?

Jibu: Jina la kwanza linalonijia kichwani ni Diamond lakini nikimfikiria Rayvanny chaguo langu linaenda kwake yeye na kwangu mimi ndiye msanii bora wa siku zijazo wa Tanzania. Ana sound ya kidunia ya sasa lakini pia tayari amechukua tuzo kubwa ambayo hakuna msanii mwingine amechukua.

Swali: Kufanya kazi kwenye muziki wako nje ya Afrika kuna changamoto kwako?

Jibu: Hakika, hapa muziki maarufu zaidi ni Hip Hop. Kwa hivyo kujaribu kutafuta mahali hapa ni changamoto kubwa kwangu kwa sababu niko katika aina ya majaribio. Nashangaa ni aina gani ya Afro inaweza kunitengenezea hadhira katika jamii hii ambayo najua nusu ya kanuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents