Hospitali ya kanisa KCMC yajiimarisha zaidi kwa upasuaji

BAADA ya kupata mafanikio makubwa katika upasuaji mkubwa wa moyo, Hospitali ya Rufaa ya KCMC sasa itaendesha operesheni ya kurekebisha mdomo uliopasuka,fizi na na paa la ndani.

Na Daniel Mjema, Moshi


BAADA ya kupata mafanikio makubwa katika upasuaji mkubwa wa moyo, Hospitali ya Rufaa ya KCMC sasa itaendesha operesheni ya kurekebisha mdomo uliopasuka,fizi na na paa la ndani.


Taarifa ya KCMC iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana mjini Moshi ilisema operesheni hizo zitaendeshwa na wataalamu bingwa wa upasuaji wa KCMC kwa kushirikiiana na wenzao kutoka nchini Hispania.


Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Huduma za Hospitali wa KCMC, Dk Mark Swai,upasuaji huo utaanza Januari 14 hadi Januari 19 mwaka huu katika Hospitali hiyo inayomilikiwa na Shirika la Msamaria Mwema(GSF).


“Tunawaomba wenye matatizo haya kuanzia watoto hadi watu wazima wafike KCMC kwa lengo la kurekebisha sehemu hizo muhimu ili kuwawezesha kuishi bila ulemavu wa aina hiyo,” alisema Dk Swai.


Dk Swai alisisitiza kuwa upasuaji huo utawahusu wale tu walio na midomo iliyopasuka, fizi na paa la nsani uliosababishwa na ugonjwa tangu kuzaliwa kwake na kuwataka kuripoti KCMC siku moja kabla ya upasuaji kuanza.


KCMC imekuwa ikipongezwa na watanzania walio wengi kutokana na kupata mafanikio makubwa katika upasuaji wa moyo kwa awamu ambao ulihusishwa madaktari bingwa wa KCMC na wale kutoka Nchini Marekani.


Tangu KCMC ianze kufanya upasuaji huo,imefanikiwa kuokoa zaidi ya Sh300 Milioni ambapo kama wagonjwa zaidi ya 50 waliofanyiwa operesheni wangelipa gharama halisi basi gharama ingekuwa ni ya mamlioni.


Mathalani kwa wagonjwa 43 waliofanyiwa upasuaji KCMC walichangia jumla ya Sh4.4 milioni tu kati ya Sh229.2 milioni ambazo ndizo zilizopaswa kuwa gharama halisi za kuwafanyia upasuaji wagonjwa hao.


Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents