Burudani

Huu ndio mkwanja aliotumia Rose Ndauka kuisimamisha Ndauka Music

Ni siku chache tu zimepita baada ya kushuhudia utambulisho wa label mpya ya muziki, Ndauka Music inayomilikiwa Rose Ndauka. Uzinduzi wa label hiyo ulienda sambamba na kutambulishwa kwa msanii wake mpya Casso, sambamba na wimbo wake, Kitonga ambao umeshaanza kuchezwa kwenye redio na TV.

14676622_1222397384449780_5639148435941621760_n

Baada ya utambulisho huo kupita hatimaye Rose Ndauka amesema mpaka sasa ameshatumia takriban shilingi milioni 20 kuisimamisha Ndauka Music.

“Mpaka hapo ilipofikia approximately nimeshatumia kama milioni 20 na.. mpaka hapa nilipofikia lakini sio kwamba hiyo ndio itakayowezesha Ndauka Music kusimama, bado tunaendelea kuinvest,” amesema Ndauka nilipofanya naye mahojiano ofisini kwake Mwenge.

Ujio wa Ndauka music unazidi kuongeza idadi ya music label hapa nchini ikitanguliwa na label kadhaa kama Tiptop Connection, Mkubwa na Wanawe, LFLG, Endless Fame, WCB, The Industry za zingine.

BY EDWARD FABIAN

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents