Fahamu

Huyu ndio Mwafrika aliyewekwa kwenye hifadhi ya wanyama kama maonyesho Marekani (+Video)

Ota Benga alitekwa nyara kule ambako sasa hivi kunafahamika kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 1904 na kupelekwa Marekani lengo likiwa nikumfanya kuwa onyesho.

Mwanahabari Pamela Newkirk, ambaye ameandika mengi kuhusu suala hilo, anaangalia matukio kadhaa ya kuficha ukweli wa kile kilichotokea.

Zaidi ya karne moja baada ya suala hilo kuangaziwa kimataifa kwa kumuonesha mwanaume kijana Mwafrika katika makazi ya nyani, Bustani ya Wanyama ya Bronx, mji wa New York hatimae imeonesha masikitiko yake.

Shirika la kuhifadhi Wanyama pori limeomba msamaha kwa onesho la mwaka 1906 la kumuonesha Ota Benga, mzaliwa wa Congo, hatua iliyokuja baada ya maandamano duniani yaliyosababishwa na video inayoonesha mauaji ya George Floyd na kuanza tena kuangazia ubaguzi unaotokea Marekani.

Wakati Marekani inakumbana na maandamano hayo, Cristian Samper, Rais wa chama cha uhifadhi wa wanyama pori, alisema ni muhimu “kuakisi historia ya hifadhi hiyo na ubaguzi wa rangi katika taasisi zetu”.

Aliapa kwamba bustani ya wanyama ya Bronx, itahakikisha kwamba inakuwa na uwazi kuhusu kile kilichogonga vichwa vya habari kote Ulaya na Marekani kuanzia Septemba 9, 1906 siku moja baada ya Ota Benga kuoneshwa kwenye onesho hadi alipoondolewa kwenye bustani hiyo. Septemba 28, 1906.

‘Alikuwa mfanyakazi wa hifadhi hiyo’

Badala ya kujikita kwenye mafunzo waliopata, Shirika hilo la uhifadhi wa wanyama pori limejihusisha na walivyoficha ukweli kwa karne nzima kipindi ambacho lilishindwa kuweka sawa au kuzungumzia kile ambacho hasa kilikuwa kimetokea kwa mwanaume huyo mweusi.

Mapema mwaka wa 1906 barua kutoka kwa hifadhi hiyo inaonesha kwamba wakati ukosoaji wa kitendo hicho unaendelea, maafisa waliamua kuanzisha taarifa za uongo kwamba Ota Benga alikuwa mfanyakazi wa hifadhi hiyo.

2px presentational grey line

Ota Benga alikuwa nani?

  • Alikamatwa Machi 1904 na mfanyabiashara wa Marekani Samuel Verner kutoka kule ambako kulikuwa kunafahamika kama Congo ya Ubelgiji. Umri wake haujulikani, pengine alikuwa na miaka 12 au 13
  • Alisafirishwa kwa meli hadi New Orleans na baadae mwaka huo aliwekwa kwenye maonesho ya Dunia huko St Loius na vijana wengine wanane
  • Maonesho hayo yaliendelea hadi miezi ya baridi ambapo kundi hilo halikupewa nguo za kujikinga na wala malazi.
  • September 1906, aliwekwa kwenye maonesho kwa siku 20 katika bustani ya wanyama ya Bronx huko New York na kuwa kivutio cha wengi kufika katika eneo hilo.
  • Ghadhabu kutoka kwa mawaziri wa Kikristo ilitamatisha kushikiliwa kwake na alihamishwa hadi hifadhi ya yatima weusi ya Howard New York iliyokuwa inasimamiwa na mchungaji Mmarekani Mweusi James H Gordon.
  • Januari 1910 alienda mji wa Lynchburg. Seminari ya kitheolojia kwa wanafunzi weusi huko Virginia.
  • Huko alifunza wavulana waliokuwa jirani namna ya kuwinda na uvuvi pamona na kuwasimulia kilichomtokea nyumbani.
  • Baadae alisemekana kwamba amepata ugonjwa wa sonona kutokana na kutamani nyumbani kwao na Machi 1916 akajipiga risasi kwa bunduki ambayo alikuwa ameificha. Inadhaniwa kwamba wakati huo alikuwa na umri wa karibu miaka 25.

Chanzo: Spectacle: Maisha ya kushangaza ya Ota Benga)

2px presentational grey line

Mwaka 1916, baada ya kifo cha Benga, makala ya gazeti la New York ilifuta simulizi ya maonesho yake.

“Kazi hii ndio chanzo cha kujulikana kwa taarifa ambayo ilikuwa iliyofichwa na hifadhi ya wanyama pori kuwa alikuwa akishikiliwa kwenye hifadhi kama mmoja wa waliokuwa wakifaniwa maonesho kwenye kizimba cha nyani. Makala hayo yameeleza.

A photo of four Africans, including Ota Benga on the right, taken in 1904 during the World's Fair in St Louis
Ota Benga (kulia) akipigwa picha katika maonesho ya Dunia ya mwaka 1904 ambapo yeye na wenzake walioneshwa kama “Mbilikimo”

Makala hayo ilikinzana na nyingine nyingi zilizotolewa miaka kumi ya awali katika magazeti mbalimbali kote nchini humo na Ulaya.

Gazeti la New York Times pekee lilikuwa limechapisha taarifa kadhaa kuhusiana na suala hilo, moja wapo ikiwa ni Septemba, 9 1906, ambayo kichwa cha habari kilikuwa: ” Bushman Shares A Cage With Bronx Park Apes”. Yaani ‘Mtu wa porini aishi na nyani kwenye kizimba kimoja kwenye hifadhi ya Bronx’

Kisha, mwaka 1974, William Bridges, mtunzi wa hifadhi hiyo alidai kwamba huenda kile hasa kilichotokea kisifahamike.

‘Urafiki kati ya aliyetekwa nyara na mteka nyara’

Kulikuwa na kitabu kilichochapishwa 1992 na mwandishi mwenza alikuwa mjukuu wa Samuel Verner, mwanaume aliyekwenda Congo akiwa amevalia mavazi ya kijeshi kumteka Ota Benga na wengine kwa ajili ya maonesho ya dunia mwaka 1904 huko St Louis.

Cha kushangaza, kitabu hicho kiliashiria uhusiano wa kirafiki kati ya Verner na Ota Benga.

Katika moja ya magazeti tangu kuchapishwa kwa kitabu hicho, lilionesha kwamba kijana Verner pia alidai kuwa Ota Benga – ambaye alipinga vikali kukamatwa kwake – alifurahia kuwa kama onesho huko New York.

The entrance to the Bronx Zoo pictured in 2016
Shirika la Uhifadhi wa Wanyama, linaloendeshwa na Bronx Zoo, limesema linashutumu baadhi ya historia iliyotolewa

Hifadhi ya wanyama sasa imeweka taarifa mtandaoni miongoni ikiwa ni barua zenye taarifa za maisha ya kila siku za Ota Benga na mwanaume aliyemteka nyara.

Miaka mitano tangu kuchapishwa kwake, maafisa wa hifadhi ya wananyama walikataa kuomba msamaha kwa kitendo hicho au hata kuzungumza na vyombo vya habari.

Na mwanahabari Pamela Newkirk alipopata fursa ya ya kutembelea eneo ambapo Benga alikuwa amefanywa kuwa onesho, jengo hilo limefungwa kuuzuia Umma.

‘Nyumba nzuri kwenye makazi ya nyani’

Sasa, Cristian Samper, Rais wa chama cha uhifadhi wa wanyama pori amesema “Tunasikitika kwamba watu wengi na vizazi vimeumizwa kwa matendo haya au kwa kushindwa kwetu kukemea kitendo hicho hadharani na kwa wakati ufaao.”

Ota Benga pictured in 1904
Ota Benga na wengine walitekwa na kupelekwa Marekani kwa ajili ya maonesho ya dunia mwaka 1904 huko St Louis.

Aidha, Bwana Samper hakumtaja William Hornaday, mkurugenzi wa hifadhi hiyo ambaye pia alikuwa mwanzilishi wa Hifadhi ya Wanyama ya Washington.

Hornaday alikuwa amejaza chumba cha Ota Benga mifupa kuashiria kwamba wala watu na wanyama na kusema kwamba Ota Benga alikuwa na “makazi mazuri sana katika nyumba ya nyani”.

Tukio hilo ni fursa kwa shirika la hifadhi ya wanyama kuelimisha Umma kuhusu historia ya yaliyotokea.

Na pia kumekuwa na mapendekezo kwamba moja ya taasisi inafikiria kujipa jina la Ota Benga ambaye maisha yake ya kusikitisha yana uhusiano mkubwa na Bustani ya wanyama pori.

https://www.instagram.com/tv/CHcrF7yhY_G/

https://www.instagram.com/tv/CHcrF7yhY_G/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents