Burudani

Ifahamu sababu ya Ne-Yo kuvaa kofia muda wote, tazama picha zake bila kofia

Umeshawahi kujiuliza kwanini muimbaji wa R&B wa Marekani, Ne-Yo huwa haachi kuvaa kofia kila anapoonekana? Ipo sababu ya kufanya hivyo.

Ne-Yo1

Ne-Yo ambaye yupo nchini Kenya kushiriki kwenye kipindi cha Coke Studio Africa, alikutana na swali la huwa anaficha kitu gani chini ya kofia yake?

Ne-Yo n Kiba

Alianza kujibu kwa utani “Nilipokuwa mdogo, nilipata ajali mbaya sana-Natania” akaendelea “Ni kichwa tu. Ni kikubwa kupita kawaida lakini tofauti na hapo ni kichwa tu”.

“WHEN I WAS YOUNG, I GOT IN A REALLY BAD ACCIDENT- JUST KIDDING. IT’S JUST A HEAD.IT’S A LITTLE BIGGER THAN AVERAGE BUT OTHER THAN THAT IT’S JUST A HEAD” Ne-Yo alimjibu mwandishi wa Mpasho.co.ke.

Ne-yo bila kofia-3
Ne-Yo bila kofia

Ne-Yo aliwahi kusema kuwa sababu kubwa ya kuvaa sana kofia alikuwa akizomewa shuleni kutokana na kuanza kuwa na ‘upaa’ akiwa mdogo sana.

“nilianza kuvaa kofia nilipokuwa mdogo sana nikiwa high school.” Maneno ya Ne-Yo kupitia post ya Thisis50.com ya mwaka 2010.

Ne-yo bila kofia-2

“Wanaume wote katika familia yangu walianza kupoteza nywele zao wakiwa wadogo sana. Nilianza kupata upaa nikiwa na miaka 15 na unajua watoto wa high school walivyo watundu, so nilianza kuvaa kofia kwa sababu hiyo.”

Aliongeza kuwa toka wakati huo amezoea kuvaa kofia kiasi kwamba asipovaa anajiona kama yupo uchi.

“But then as time progressed and I started developing my thick skin it didn’t really matter anymore what people thought, but at that point a hat felt normal. Now I feel naked without one.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents