BurudaniHabari

Ijumaa ya Bongo Fleva, Marioo, Harmonize na Rayvanny wana matukio siku moja

Siku ya Ijumaa hii itakuwa siku ya Kibongo Fleva zaidi kwani kutakuwa na matukio matatu makubwa amabyo yatakuwa chini ya wasanii watatu pia wakubwa wa muziki wa Bogo Fleva.

Baada ya Marioo kuwa msanii wa kwanza kutangza kuwa tarehe 12/05 Ijumaa hii atakuwa na event yake ya kutambulisha THE KLID YOU KNOW DELUXE EDITION ikiwa kama muendelezo wa Album ya THE KID YOU KNOW.

Siku kadhaa naye Harmonize akatangaza kuachi ngoma yake ya Zanzibar Ijumaa hii ya tarehe 12/05 ambayo amesha shoot mpaka video na jana alieleza historia fupi kuwa ndio ngoma iliyosababisha akamatwe Zanzibar na kulipishwa faini baada ya kushoot video haliyakuwa ni mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Siku za nyuma Rayvanny alitangaza kuwa ataachi Tracklist yake ya Flowers III,  na hii ni baada ya kuchaia Flowers I na Flowers II ambazo zote zimefanya vizuri sana.

Tarehe ya kuiachia Flowers III naye ametangaza kuwa ni Ijumaa hii ya Tarehe 12/05.

Ijumaa hii tunaiita Ijumaa ya Bongo Fleva.

Unahisi siku itakuwa kubwa kwa msanii gani??

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents