Burudani

Irene Uwoya kufanya kolabo tu ahitaji Tsh. Milioni 27, Dogo Janja aahidi kuzama mfukoni

Mara kadhaa zimesikika stori za Dogo Janja kufanya kolabo na mkewe, Irene Uwoya, sasa msanii huyo amefunguka kipi kinaendelea.

Dogo Janja amesema kuwa wazo la kufanya ngoma pamoja analo toka siku nyingi ila Irene amemueleza ili kufanya hivyo anahitaji kulipwa Dola za Kimarekani 12, 000 (zaidi ya Tsh. Milioni 27).

“Mpaka sasa hivi bado hatujafikiana muhafaka wa fedha, anataka kiasi kikubwa ila nyingi sana, US Dollar 12,000 ndio anayotaka atie sauti, namtafutia nampa,” Dogo Janja ameiambia Clouds FM.

Soma Pia: Dogo Janja na Irene Uwoya katika muziki: Madee afunguka (+Video)

May 02, 2018 katika mahojiano na Bongo5, Madee alisema kolabo ya Dogo Janja na Irene Uwoya ni project ambayo bado haipo rasmi lakini ni wazo ambalo aliletewa na akaona ni zuri kibiashara ila hakuna chochote kilichofanyika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents