Burudani

J. Cole, Wizkid na Davido kupanda jukwaa moja

Msanii wa muziki kutoka Marekani J.Cole  anatarajiwa kutua nchini Nigeria ifikapo Mwezi April mwaka huu katika tamasha kubwa la muziki.

J.Cole anatarajiwa kutoa burudani katika jukwaa la Castle Lite Nigeria‘s Castle Lite Unlook litakalomkutanisha na wakali wa muziki kutoka nchini humo ambao ni Wizkid na Davido.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika  April 27, 2018 katika ukumbi wa Eko Hotel & Suites jijini Lagos.

Mnamo mwaka 2017 mwezi Julai, waandaji wa Tamasha hili walimdondosha msanii wa Hip Hop kutoka Marekani, Future na msanii kutoka Afrika Kusini, Caspanyovest katika ardhi ya Tanzania kutoa burudani.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents