Habari

Jaji Warioba amjibu Kingunge “tusimbebeshe mzigo Rais”

Waziri mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema viongozi wakuu wastaafu ambao ni Marais na mawaziri wakuu wamekuwa wakimshauri rais katika masuala mbalimbali lakini sio katika vyombo vya habari.

warioba

Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale-Mwiru aliwataka Marais wastaafu na Mawaziri Wakuu wastaafu nchini kuingilia mvutano wa kisiasa unaoendelea.

Warioba amemjibu Kingunge akisema,”Kweli tuko kimya lakini ukimya huo usitafsiriwe vibaya kuwa hatumshauri Rais Magufuli, sisi kama viongozi wastaafu tunamshhauri rais lakini sio katika vyombo vya habari.”

“Badala ya kumjibu Kingunge ni vyema kumuachia Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi awakutanishe viongozi wa vyama vya siasa kujadili hali hiyo kwa lengo la kupata muafaka”, aliongezea.

“Ni wajibu wa Watanzania wote kuhakikisha wanalinda hali ya amani nchini badala ya kuliona jambo hilo, na kusema jambo hili halimhusu Rais John Magufuli pekee linamhusu mtu mwingine yeyote. Tumsaidie msajili katika hili, hili sio tatizo la mtu mmoja bali ni la nchi nzima, tusimuachie Rais wetu.”

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents