Jamaica yafanya kweli taji la urembo Miss Dunia

Shindano la Miss World 2019 limefanyika kwa mara ya 69 usiku wa kuamkia leo Disemba 15, 2019 katika Ukumbi wa ExCeL London Jijini London, Uingereza ambapo mrembo wa Jamaica Toni-Ann Singh ametwaa taji hilo la ulimbwende la Dunia.

Mrembo wa Dunia 2019/2020 kutoka nchini Jamaica, Toni-Ann Singh.

Shindano hilo la ulimbwende lilikutanisha warembo kutoka Mataifa mbalimbali duniani, ambapo nchi ya Tanzania iliwakilishwa na Mrembo Sylvia Sebastian Bebwa, ambaye yeye kwa juma lililopita aliingia katika 20 bora ya warembo wenye vipaji, baada ya yeye kuonesha kipaji cha kucheza ‘Robot Dance’.

IMG_3102.JPG

Mbali na Urembo, Mlimbwende huyo wa Dunia anapenda kutoa Elimu ya afya ya akili na matarajio yake ni kuwa Daktari na taji lake amelipokea kutoka kwa Venessa Ponce De Leon, Mrembo kutoka nchini Mexico alitwaa taji hilo mwaka 2018.

Katika mashindano hayo mshindi wa pili alikuwa mrembo kutoka Ufaransa, Ophely Mezino, wa tatu ni Suman Rao kutokea nchini India

IMG_3101.JPG

Singh ana umri wa miaka 23 na ni mhitimu Chuo Kikuu cha Florida alipokuwa akisoma masomo ya saikolojia na wanawake.
Image result for Toni-Ann Singh
Hii ni mara ya nne kwa Jamaica kupata taji hili na mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1993. Kabla ya hapo ilichukua taji hilo mwaka 1963 na 1976.

Related Articles

Back to top button