Habari

Jambazi aliyekutwa na silaha auwawa akitaka kutoroka Msasani Dar (Video)

Jeshi la polisi kanda maalum limefanikiwa kumuua jambazi mmoja aliyefahamika kwa jina la KILAMBO OBALE@NYASAIRO miaka 44, mkazi wa Chanika.

Mnamo tarehe 27/05/2021 majira ya saa tano usiku, mtuhumiwa huyo alikamatwa kwa makosa ya kujihusisha na matukio ya ujambazi katika mkoa wa Mara na Dar es salaam.

Baada ya mtuhumiwa huyo kuhojiwa alikiri kujihusisha na matukio hayo na anamiliki silaha, Hivyo askari walimwamuru kwenda kuonesha silaha hiyo ilipo na wakati askari na alipofika eneo a silaha alipofukia ardhini silaha hiyo walianza kuchimba ndipo mtuhumiwa alikurupuka na kukimbia kuingia kwenye maporomoko ya kingo za baharí.

Askari walipiga risasi hewani ili kumwonya asimame lakini hakutii na aliendelea kukimbia na hivyo askari walimpiga risasi kwenye mguu wa kulia na akaanguka chini. Mtuhumiwa alifariki dunia wakati anapelekwa Hospitali ya Mwananyamala.

Askari waliendelea kuchimba eneo aliloonyesha na kufanikiwa kuipata Bunduki aina ya S/GUN yenye namba S/NO.006074010/CAR 00097133.

Katika uchunguzi wa awali inaonyesha kuwa mnamo tarehe 23/04/2021 mtuhumiwa huyo akiwa na washirika wake walivamia nyumbani kwa Capt. MILTON LUSAJO LAZARO, Mstaafu wa JWTZ, Mkazi wa Masaki Dar es salaam na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo TV aina ya LG inchi 49, Laptop aina ya Mac Book air na fedha za CANADA dola 2700 pamoja na silaha hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents