Jambo Jambo ya Steve RnB inatoa muelekeo mzuri wa Tanzania kufanya reggae ya kisasa

http://www.youtube.com/watch?v=Uzs9C8aF_Y0

Kama umepata fursa ya kuona video ama kusikiliza wimbo mpya wa Steve RnB Jambo Jambo utakubaliana nasi kuwa msanii mwenye ladha ya R&B akiimba reggae huzalisha wimbo wenye melody nzuri sana. Infact, reggae ya sasa ndivyo ilivyo. Ni mchanganyiko wa R&B na beat ya reggae yenye vionjo vya kuvutia zaidi.

Kwa Jamaica pamoja na kuendelea kuwepo kwa wasanii wa muziki huo wanaoimba reggae asili, siku za hivi karibuni wameibuka wasanii wengine wenye ladha ya R&B zaidi.

Huwezi kuacha kuwataja watu kama Busy Signal, Daville, Christopher Martin, Cecile, Alaine na wengine. Muziki huo umeboreshwa zaidi kwa kuwepo mfumo wa ‘riddim’ ambapo beat moja ya reggae huweza kutumiwa na hata wasanii 10 huku kila mmoja akiimba ujumbe wake mwenyewe na ladha tofauti. Hiyo ndio imemfanya Steve R&B afikirie kutumia riddim iliyotumia pia na Busy Signal kwa wimbo wake Missing You.

Kama aliota vile, sasa Jambo Jambo ya Steve imetokea kupendwa mno na wapenzi wa muziki. Na kwa uhakika kabisa Steve ameonesha mustakabali mzuri wa kuja kuwa mwanamuziki bora wa reggae ya kisasa. Jambo Jambo is such a nice tune. Big up Steve.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents