Burudani

Janet Jackson na mumewe wapata mtoto wa kiume

Mwanamuziki mkongwe nchini Marekani Janet Jackson hatimaye amejifungua mtoto wa kiume akiwa na umri wa miaka 50, afisa wake wa mawasiliano amethibitisha.


Mwanamuziki Janet Jackson na mumewe, Wissam al-Mana

Taarifa imesema mwanamuziki huyo na mumewe Wissam Al Mana, ambaye ni mfanyabiashara kutoka Qatar, wana furaha kumpata mtoto wa kiume waliyempa jina Eissa Al Mana.

“Janet alijifungua bila matatizo yoyote na kwa sasa anapumzika,” afisa wake amesema. Watu walianza kushuku kuwa alikuwa ameshika mimba Aprili mwaka jana alipoahirisha ziara yake ya kutumbuiza ya Unbreakable.

Alipakia video kwenye Twitter wakati huo na kuwaambia mashabiki kwamba alikuwa anaahirisha ziara hiyo “kwa sababu kulitokea mabadiliko ya ghafla”.

“Nilifikiri ni muhimu sana kwenu kuwa wa kwanza kufahamu hili,” alisema, na kuongeza: “Tafadhali, naomba mjaribu kunielewa kwamba ni muhimu sana nilifanye hili kwa sasa.”

Alisema alitaka kuangazia kuunga familia na mumewe, ambaye walifunga pingu za maisha mwaka 2012. Awali Jackson alikuwa ameonekana akinunua nguo na vitu vingine vya kutumiwa na watoto London.

Janet Damita Jo Jackson alizaliwa 16 Mei 1966 mjini Gary, Indiana, ndiye mtoto wa mwisho miongoni mwa watoto tisa wa familia yake na ni dadake nyota wa muziki wa Pop marehemu Michael Jackson.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents