Burudani

Jay-Z amchimba mkwara Chris Brown: ‘Hurt Rihanna and I’ll Finish You’

Imedaiwa kuwa bosi wa Roc Nation, Jay-Z alimchimba mkwara Chris Brown backstage wakati alipohudhuria show yake ya Barclays Centre akiwa na Rihanna.

“Jay-Z alimwambia Rihanna kuwa kama Chris anakufanya uwe na furaha basi kuwa naye” chanzo kimoja kililiambia gazeti la The Sun..

“Aliwaalika kama ‘couple’ kwenye concert yake jijini New York na akiwa backstage alimuita Chris pembeni na kumwambia kuwa kama akimuumiza Rihanna, iwe kimwili ama kihisia ndo mwisho wake,” kiliongeza chanzo hicho.

Kuna tetesi kuwa Rihanna na Chris – aliyemwacha mpenzi wake Karrueche Tran, wana mpango wa kuutangaza uhusiano wao kwa umma mwezi ujao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents