BurudaniUncategorized

Jay Z kuwaona mapacha wake

Rapa Jay Z ameonekana akitabasamu baada ya kuwasili kutokea West Hollywood alipokuwepo na huwenda safari yake ikaonganika hadi hospitalini kumcheki babay mama wake Beyonce aliyejifungua watoto mapacha.

Jay ambaye kwa sasa ametua katika jiji la Los Angeles, baada ya mizunguko aliyokuwa nayo ikiwemo ule wa Jamaica alikoenda kufanya project katika studio za Damian Marley ikiwa ni moja ya maandalizi ya albamu yake inayokuja.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Beyonce anadaiwa kujifungua mapacha wa kike na wa kiume, wiki moja kabla ya habari kuzagaa siku ya Jumapili.

Hata hiyo Beyonce bado yupo katika uangalizi maalumu kwenye hospitali na huwenda naendelea vizuri, kwani Jay Z amenekana mwenye bashasha la kuashiria kuwa familia yake iko sawa kabisa.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents