Burudani

JB aeleza kinachomnyima usingizi katika filamu

Mwigizaji na mwongozaji wa filamu, Jacob Stephen aka JB amesema tatizo linalomnyima usingizi katika tasnia ya filamu ni kukosa waandishi wazuri wa miswaada.
11849077_419311034935419_1542595592_n

Kupitia ukurasa wa instagram wa JB ameandika : Tasnia yetu ya filamu inakabiliwa na changamoto mbalimbali lakini kwangu mimi changamoto kubwa kuliko zote inayoninyima usingizi ni waandishi wa miswaada (script). Hili kwangu ndio tatizo kubwa kuliko yote, mfano natarajia kufanya filamu yangu na King Majuto toka mwaka jana mwezi wa 8 mpaka leo sijafanya, kati ya script 10 nilizoletewa hakuna inayofaa. Wapo wapi waandishi??? niko tayari kununua kwa bei yoyote. Lakini ukiniletea kituko tarajia ngumi kama malipo ya usumbufu ndo maana tangu nitoe Mzee Wa Swaga mwezi wa pili mpaka leo sijatoa nyingine. Malighafi (script) hamna.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents