Habari

Je upo kwenye mahusiano yenye manyanyaso? Kunyamaza sio suluhisho

Je unaingia gharama gani kwenye mahusiano hayo? Kama ni kufikia ndoto za maisha yako, utu wako na mwonekano wako gharama ni kubwa. Inawezekana uko na jamaa makini kwa mwonekano wa nje. Alikuwa msikivu, mpole na mwerevu mpaka unaingia kwenye mahusiano hadi kufunga ndoa hakuna tatizo kabisa na wala hutaweza kushitukia kwamba huyu jamaa ni mnyanyasaji na katili kwenye mahusiano.

Domestic violence

Unakuja kushangazwa na makofi na matusi mara utakapofika ndani na unajaribu kujiuliza huyu mtu kabadilikia wapi? Ukweli wa mambo hakuna kilichobadilika ni namna tu wewe ulipokuwa kwenye mahusiano ulimwangalia au kumchunguza kutoka sura ipi, vitu vingine ulivipotezea kwa namna alivyokuwa anaonekana kukujali hadi ukashindwa kufanya uchunguzi wa utu wake halisi ni upi?

Makala hii inahusu tu wale ambao wanahitaji kujenga maisha ya baadaye na wenza wao. Kama wewe ni kiruka njia na wala huna mpango unapoingia kwenye mahusiano na watu wengine potezea tu.

Ukweli ni kwamba huwezi kujua ukatili wa mtu kwa kumwangalia kwa nje tu, kuna baadhi ya vitabia ambavyo hutakiwi kuvipotezea;

Huwa hawajiamini kabisa Watu hawa ukiwaangalia kwa nje ni watemi,shujaa na wanaonekana kujiamini ila ndani ya mioyo yao hakuna kitu kama hicho. Hisia zao ni nyepesi sana, hivyo huhitaji watu wengine ili kuonekana jasiri na woga wa kuhofia kumpoteza mtu aliyenaye kwenye mahusiano anaona ni bora awe anamtawala kila kona. Kutokana na hali ya kutawala kila kitu hufanya vitu fulani ambavyo atakwambia kwanini anafanya hivyo, ni kwamba atasema ni kwasababu anakujali sana ndio maana anafuatilia kila hatua unayopiga, watu unaoongea nao na hata watu unafanya nao kazi. Na wakati mwingine atahitaji kujua password zako za barua pepe simu nk.

Wahanga wa watu kama hawa ni kukimbilia mahusiano na kuanza kuishi pamoja nao. Huu ni ujasiri ambao dada zetu wanao kwa kiasi kikubwa wanaweza kuanza kuishi na mtu bila kujua huyu mtu ni wa namna gani na wakati mwingine kulazimika kuoana. Watu hawa kila kitu wanapeleka kibabe na kitemi huku wakiwa na wivu wa kupindukia kiasi kwamba hawapendi tena kukuona ukiwa na rafiki zako au familia yako. Utasikia kitu kama “hao rafiki zako angalia sana.” Huwa hawana imani wala hawawezi kukwamini. Kitu ambacho wanashindwa kujua mahusiano bila kuaminiana ni sawa kusukuma gari lililozimika kuelekea mlimani na unategemea litawaka uendelee na safari.

Watu wakatili au wenye manyanyaso kwenye mahusiano hutegemea kwamba huyo aliyenaye anatakiwa kukidhi haja ya kila kitu anachotaka. Kutokana na hali hiyo unapojiingiza kwa mtu huyo usilete habari za marafiki au familia hataki utumie muda na hao watu ila yeye tu.

Hawajui kuwasiliana hawa watu hawawezi kuonyesha hisia zao au kuongelea hisia zao, huwa wanaonyesha kuwa si dhaifu au hawana uhitaji sana kihisia. Kutokana na kutojua namna ya kuwasiliana hutumia ubabe wao au manyanyaso kupata wanachokihitaji kwa wenzi wao. Wengine hutumia kileo ili kukamilisha haja ya kuongea au kuonyesha hisia zao ndipo wanapopata ujasiri wa kuongea na mara nyingine kulazimisha mambo na baadaye kusingizia kinywaji.

Hulaumu wengine kwa matendo yao Mara nyingi watu katili hufanya ukatili huo kwa kusingizia watu wengine, husema kuwa huyu mtu amenisababishia hasira kali ndio mana nimempiga au kumfanyia hivi. Kwani ni mara ngapi wahanga wa matukio haya kusikia maneno kama “kwanini umenifanya nifanye hivi? ni ujinga jinga wako unaoufanya”.

Ni waigizaji wazuri Watu katili kwenye mahusiano wanachokionyesha mbele za watu ni tofauti sana na kinachotokea kwenye nyumba zao. Kazini wanasifika kwa utu na kuchapa kazi na wana marafiki wengi na ndugu wengine huwapenda pia. Lakini unapofika kwa mkewe ni vitu viwili tofauti sana na hata huonyesha ukatili kwa watoto.

Je unafanyaje Sasa?
Fanya kila jitihada mahusiano hayo yafanye kazi, inawezekana mwenzio hajui kwamba hilo ni tatizo. Kama anajali uhusiano huo atakuwa tayari kubadilika na vilevile mmwone mshauri wa mambo ya mahusiano na ndoa.

Tabia yako ya kunyamaza inaweza kumfanya mwenye tabia hiyo aendelee nayo, simama uongee na ujiteteee usije ukafa siku si zako.

Je inakugharimu kiasi gani kuwa kwenye mahusiano hayo ambayo yana ukatili na unyanyasaji? Kama jibu lako ni sababu ya kutimiza ndoto za maisha yako, au watu wakuone una maisha fulani itakubidi ulipe gharama. Chanzo ni kutoka kwa mwanasaikolojia!

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents