Burudani

Julio (BBA) adai amesharekodi nyimbo 80 ‘nina mzigo wa kutosha’

Aliyewahi kuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa, Julio Batalia anataka watu wafahamu kuwa hafanyi muziki kwa kujaribu. Rapper huyo amedai kuwa mpaka sasa amesharekodi nyimbo 80.

julio haya

Julio amedai anajituma kufanya muziki kwakuwa jukumu la kuufikisha muziki wa Tanzania kimataifa ni la kila msanii na si wasanii wachache.

“Wasanii sasa hivi tunatakiwa kuacha kuuchukulia muziki wetu poa. Kama umefanya muziki wako, jitahidi na kufanya na video kali sana ili kuuweka muziki kwenye standard moja,” ameiambia Bongo5. “Unajua inaonekana kuna wasanii wachache ambao wanautia thamani muziki wao, kwahiyo mimi nahakikisha katika ngoma zangu 80 ambazo zipo tayari, natoa kitiming, ngoma niliyofanya November ninaweza kuitoa December au January au nikaichunia nikatoa ngoma ya mwaka uliopita. Nitahakikisha kwamba natoa ngoma katika mazingira ya album. Kwahiyo watu na wadau wa muziki wangu waendelee kufuatilia muziki wangu kwa makini kwani sasa hivi niko vizuri na nina mzigo wa kutosha.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents