Bongo5 ExclusivesBurudaniHabariMahojiano

Juma Lokole kuhusu kuiba stori za Mange kuzitumia WasafiFm

Mtangazaji wa WasafiFM Juma Lokole ni mtu wa karibu sana na Paula lakini pia Diamond ni Boss wake, amezungumza na @el_mando_tz juu ya Boss wake Diamond kuhusishwa kutembea na Paula haliyakuwa alikuwa na Rayvanny.

Juma Lokole pia ameweka wazi kuwa kwa sasa Tanzania Sweetheart ni Paula na taji hilo ameachiwa na Wema Sepetu, ameonngeza Wema Sepetu amestaafu na Watanzania wamemvika Paula taji hilo.

Lokole ameulizwa kuhusu ugomvi wa Rayvanny na Paula na kuleza kuwa kwake yeye kama mtu wa karibu wa Paula amefurahi sana Paula kuachana na Rayvanny maana Rayvanny alitaka kumfanya Paula kama Wife Material wakati Paula sio mambo yake.

“Hata ule ugomvi wao mimi ndio nnilikuwa na simu ya Paula na nilikuwa naandika mimi Paula alikuwa ananipa za ndaani halafu mimi natafuta cha kuandika, alikuwepo mimi, Marioo na Paula mwenyewe”

Mbali na hilo Juma Lokole amefunguka pia sakata la kipindi chao cha Mashamusham kutajwa na Mannge Kimambi kuwa wanaiba story (Umbea) wake na kuutumia kwennye kipindi chao pale Wasafi media.

Mlengwa haswa alikuwa Juma Lokole na Mange alimtaja na kumshtakia kwa Diamond, @el_mando_tz amezungumza na Juma Lokole kuhusu sakata hilo.

msikilize Lokole akitoa majibu.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents