Videos

Kamanda Sirro: Tumefungua jalada kuwasaka mashoga vinara (Video)

Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema tayari wameshafungua jalada kwaajili ya kuwasaka mashoga vinara jijini Dar.

Hatua hiyo imekuja baada ya Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangallah kuagiza mashoga maarufu, James Delicious, Kaoge Mvuto na Dani Mtoto wa Mama ‘wafike wenyewe Central Police Dar es Salaam kwa mahojiano kabla hawajatafutwa.’

“Sisi tumefungua jalada tumewatafuta, lakini mpaka sasa ninapozungumza sijapata taarifa ya mtu kukamatwa. Wengine wamejitangaza kwenye mitandao, wengine wanajiita Precious sijui, ni hatari sana. kwa sababu wameshajitangaza na ukiangalia kwenye Instagram wanaonekana, wawe wasamaria wema tu waje maana yake hawana ujanja,” alisema Kamanda Sirro wakati akiongea na waandishi wa habari.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents