Siasa

Kamati ya Maadili ya Bunge yapendekeza adhabu kwa Jerry Silaa

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imetoa azimio kuhusu shauri la mbunge wa Ukonga Jerry Silaa asimamishwe kuhudhuria mikutano miwili mfululizo ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa

Akisoma azimio hilo leo Agosti 31, 2021 bungeni, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka ambaye ni mbunge wa Tabora mjini amesema mbali na kusimamishwa pia aondolewe kwenye uwakilishi wa bunge la Tanzania katika bunge la Afrika.

”Kamati ilimhoji Mh. Jerry Silaa ili kuthibitisha kauli yake kuwa mishahara ya wabunge haikatwi kodi na aliuzwa iwapo mshahara wake unakatwa kodi au haukatwi alisema kuna sehemu inakatwa kodi na kuna sehemu haikatwi kodi” – Emmanuel Mwakasaka, Mkiti kamati ya Maadili.

Mwakasaka ameongeza kuwa, ”Katika mahojiano Mh. Jerry Silaa alikiri kuwa kauli zake zimeleta tafrani kwenye jamii, uchambuzi wa ushahidi wa sheria kwenye shauri hili unathibitisha kuwa alikuwa na nia ovu ya kulidharau na kulidhalilisha bunge pamoja kuchonganisha bunge, serikali, uongozi wa bunge na wananchi”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents