Siasa

Kamati ya Maadili ya Bunge yapendekeza adhabu kwa Gwajima

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imetoa azimio la kutaka Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima kutohudhuria mikutano miwili ya bunge mfululizo.

Azimio hilo limetolewa leo Agosti 31, 2021 bungeni na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka ambaye ni mbunge wa Tabora mjini.

”Kamati ilijiridhisha kuwa kauli alizotoa Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima, zinadhalilisha bunge, zinaonesha dharau na kushusha hadhi na heshima ya bunge, shughuli za bunge na uongozi, hivyo tunaliomba bunge kumsimamisha kutohudhuria mikutano miwili mfululizo pamoja na kumpeleka azimio kwa chama chake ili kimchukulie hatua” – Emmanuel Mwakasaka, Mkiti kamati ya Maadili.

Aidha Mwenyekiti huyo wa Kamati aliongeza kuwa, ”Moja ya jambo ambalo kamati ililiona ni utovu wa nidhamu uliokithiri kwa mbunge Josephat Gwajima na kosa kama hilo kwa mujibu wa kanuni za bunge ni mbunge asihudhurie mikutano mfululizo isiyopungua miwili au isiyozidi mitatu”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents