Habari

Kampuni ya Nestle yathibitisha ubora na uhalisia wa bidhaa yake ya Nido

Kampuni mama ya bidhaa ya maziwa ya unga ya NIDO, Nestle, hivi karibuni imethibitisha ubora na uhalisia wa bidhaa yake hii maarufu ya NIDO.

NIDO-PACK-PRESS_TIN_D-swa(1)

Hii imekuja baada ya mabadiliko ya chanzo cha upatikanaji wa maziwa haya kuhamia nchi ya Afrika Kusini, mabadiliko haya yalisababisha mkanganyiko kwa watumiaji wake wa kila siku.

Kampuni ya Nestle imewahakikishia kuwa NIDO (kwenye picha) kama ilivyo bidhaa nyingine kutoka Nestle, imetengenezwa kwa kufuata viwango vya hali ya juu kabisa vya uborana kutimiza kanuni na masharti ya uzalishaji wa bidhaa za vyakula kimatiafa na hata TFDA (mamlaka ya vyakula na madawa Tanzania).

Kampuni ya Nestle pia imewatakia watanzania wote heri ya msimu huu wa sikukuu za Krismasi na mwaka mpya ikiwashukuru na kuwataka waendelee kufurahia bidhaa zake za NIDO kwani Upendo wako ndio mafanikio ya uwapendao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents