Habari

Kampuni ya sigara yaamriwa kumlipa mjane wa mvuta sigara aliyekufa kwa kansa ya mapafu dola bil.26.6!

Kundi la waamuzi wa kesi (jury) katika mahakama ya Florida nchini Marekani limeiamuru kampuni ya sigara ya RJ Reynolds Tobacco kumlipa mwanamke aliyefiwa na mume wake kwa saratani ya mapafu dola bilioni 23.6.

guy_smoking_electronic_cigarette22

Adhabu hiyo inajulikana kitaalum kama ‘Punitive damages’ na hutolewa kuyakatisha tamaa makampuni au watu kufanya mambo mabaya huku fidia au ‘compensatory damages’ hutolewa kwaajili ya kuwalipa wahanga kutokana na kile walichokipoteza.

Hivyo uamuzi wa jury hao ni kuwa kampuni hiyo inatakuwa kumlipa mwanamke huyo na watoto wake fidia ya dola milioni 7.3 na pia dola milioni 9.6 kwaajili ya mtoto wa kiume wa mume wake aliyempata kwenye uhusiano wake wa awali huku punitive damages ikiwa ni dola bilioni 23.

Mwanamke huyo aitwaye Cynthia Robinson ni mjane wa Michael Johnson, mvutaji wa sigara aliyefariki kwa saratani ya mapafu mwaka 1996 akiwa na miaka 36. Hata hivyo, wanasheria wamedai kuwa sio rahisi fedha hizi zikalipwa. Kampuni hiyo imesema itaikatia rufaa hukumu hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents