Burudani

AT adai muziki wa Bongo Flava upo ‘ICU’

Muimbaji wa muziki wa mduara, Ally Ramadhani aka AT amesema muziki wa Bongo Flava kwa sasa upo ‘ICU’ na kudai kafurahishwa na Diamond baada ya kuachia wimbo ‘Mdogo Mdogo’ wenye asili ya mchiriku.

AT 1

AT amezungumza na Bongo5 na kuwataka wasanii wa Bongo Flava kurudi kwenye muziki wao wa mwanzo uliokuwa na uwezo wa kwenda mbali.

“Niliwaambia muziki wa Tanzania ni mchiriu, mnanda, mduara pamoja na taarab, miziki mingine ni shobo zetu tu wasanii,” amesema. “Nakumbuka nilizungumza kama sikosei, nikazungumza na baadhi ya wasanii nikasema kwamba ‘ kama Diamond siku atafanya nyimbo ya mnanda basi ndo siku atawakilisha taifa lake’ na pia nikasema sio mwenyewe hata Ali Kiba akiamua kufanya nyimbo kama ya dance ambayo walikuwa wanafanya kama akina Bichuka au mnanda kwa sababu hii ni tofauti kabisa. Mnanda ni modern ya zamani kwa sasa ni mchiriku. Kwa sasa alivyo Diamond alipaswa kutengeneza mchiriku, ndio maana unaona Mdogo Mdogo inaweza kufika mbali zaidi, kwa sababu ni muziki mpya kwenye soko la muziki wa kimataifa. Juma Nature ambaye alikuwa kwenye album ya Ugali, chini ya producer P-Funk Majani, nyimbo unasikiliza unajua huu ni muziki wa Bongo Flava ya sasa ipo ICU, hauna nguvu tena, sasa hivi tunaimba muziki ambao una asili ya Nigeria na sehemu nyingine ambayo kiukweli hauwezi kwenda kokote. Tukae kwenye asili ya muziki wetu na tuupeleke mbele zaidi,” amesema msanii huyo.

Katika hatua nyingine AT amezungumzia ujio mpya wa muziki wake ambao amedai utawashangaza wadau wake.

“Kwanza nilikuwa nasoma ramani,” ameeleza. “Nilikuwa nasoma ramani ya muziki unapokwenda, kinachofuta sasa hivi ni kitu cha ghafla, nyimbo zitazokuja sasa hivi ni tofauti na zile ambazo mlikuwa mnazisikia, ni mduara lakini ni mwingine mpya umeletwa. Kwahiyo huu mpya ndo utakaoleta mapinduzi kwenye muziki, kwa maana ni mapinduzi mara mbili kwenye muziki wa mduara. Nilikuwa niachie kazi hivi karibuni lakini nikaona bora nikimaliza Ramadhan ndo itakuwa poa. Nilitengeneza muziki wa mduara nikaona watu wengi wanafanya kama wako. Tanzania ukifanya kitu na watu wanataka kufanya kama wewe, kwahiyo mimi nimeamua kubadilisha muziki wangu kidogo kwa kuuboresha zaidi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents