Burudani

Kanye West ndiye Executive producer wa albam mpya ya Rihanna ‘R8’ iliyoko jikoni

Miongoni mwa albam zinazosubiriwa kwa hamu mwaka huu ni pamoja na albam ya nane ya Rihanna “R8” ambayo iko jikoni.

Kanye n Riri

Kanye West ameweka wazi kuwa yeye ndiye Executive producer wa album hiyo ambayo itatoka hivi karibuni. Habari hiyo ameitoa wakati akizungumza na Ryan Seacrest kwenye Red carpet ya tuzo za Grammy zilizotolewa Jumapili iliyopita.

Tayari Rihanna ametoa single ya kwanza “FourFiveSeconds” mwezi uliopita, ambayo amewashirikisha Kanye West na Paul McCartney, wimbo ambao Riri, Kanye na McCartney waliutumbuiza kwenye tuzo za Grammy.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents