HabariSiasa

Kenya yamtimua mtendaji mkuu wa Ufaransa tatizo la uhaba wa mafuta

Serikali ya Kenya imethibitisha kufukuzwa kwa mtendaji mkuu  wa Ufaransa moja ya wafanyabiashara wakubwa wa mafuta nchini Kenya kufuatia tatizo la uhaba wa mafuta.

Mtendaji mkuu wa Rubis Energy Kenya, Jean Christian Bergeron alikuwa mtu wa kwanza kuchukuliwa hatua, tangu mdhibiti wa nishati nchini Kenya kusema itawachukulia hatua wafanyabiashara wa mafuta kwa kusababisha kile inachosema ni uhaba bandia wa mafuta nchini.

Bwana Bergeron bado hajasema lolote kuhusu uamuzi wa serikali ya Kenya.

Kwa mujibu wa Wizara ya Nishati Kenya ina akiba ya kutosha ya bidhaa za petrol na uhaba huo ni matokeo ya baadhi ya wauzaji wa mafuta kuzuia na kuweka kipaumbele kusafirisha nje katika nchi jirani.

Amesema hii ni sawa na uhujumu uchumi. Waziri Monica Juma amesema serikali haitavumilia kampuni au mtu yeyote anayesababisha na kutengeneza tatizo bandia.

Serikali imesema dola milioni 295 wanazodai makampuni ya mafuta zimelipwa, wakati dola milioni 121 zilizobaki zitalipwa baadae.

Kenya imekabiliwa na uhaba wa mafuta kote nchini kwa zaidi ya wiki mbili ambao umevuruga huduma za usafiri na shughuli za kiuchumi.

Source Voice of America

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents