Habari

Kenya yatangaza kifaa kipya kitakachowabaini wanaosema uongo

Serikali ya Kenya imeamua kutumia kifaa maalum cha kuwafichukua watu watakaosema uongo dhidi ya tuhuma za ufisadi wa mabilioni nchini humo.

Miongoni mwa watakaokumbwa na mtihani huo ni maafisa wakuu wa Serikali ya Kenya ambao wametajwa katika kashfa ya mabilioni hayo yaliyokuwa mali ya Shirika la vijana wa huduma kwa jamii (NYS).

Taarifa hiyo imetolewa na Rais Uhuru Kenyatta ambaye amesema, kifaa hicho ambacho kitafichua maadili ya wafanyakazi ni miongoni mwa mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo.

Alikuwa akizungumza baada ya kufichuliwa kwa kashfa ya shilingi bilioni Nane (8) za Kenya zilipotea katika kitengo kimoja cha serikali.

Takriban wafanyakazi 40 wa umma wanakabiliwa na mashtaka hayo kufuatia kashfa hiyo.

Kashfa hiyo ya ufisadi ilifichuliwa na watoa huduma na bidhaa kwa shirika hilo ambao walikuwa hawajalipwa na kupelekea kuibwa kwa fedha hizo kupitia vyeti bandia na malipo ya ziada.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents