Burudani

Khadija Kopa kumshirikisha Diamond kufanya remix ya wimbo wa marehemu mwanaye Omary Kopa

Baada ya msanii wa Bongo fleva Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz kumshirikisha Khadija Kopa kwenye wimbo wake ‘Nasema Nawe’, malkia huyo wa mipasho ana mpango wa kumshirikisha staa huyo kufanya remix ya wimbo wa marehemu mwanaye Omary Kopa.

kopa na diamond

Kopa amesema kuwa yeye na Diamond wamezungumza na kuweka mipango ya kuurudia wimbo huo uitwao ‘Nipepee Mpenzi Wangu’ uliofanywa na mwanaye, Omary Kopa enzi za uhai wake. Omary alifariki mwaka 2007.

“Mimi na Diamond tumepanga kufanya ‘remix’ ya wimbo huo kwa kuwa mimi naujua vizuri naye anaupenda muda mrefu na amekuwa akiuimba mara kwa mara hivyo tunatumaini tutapata kitu kizuri baada ya kukamilisha kuurekodi wimbo huo,’’ alisema Kopa.

Source: Mtanzania

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents