Habari

Kijana wa Ubungo Msewe afichua siri ya kushinda tsh milioni 437 za SportPesa (Video)

YASSIN Ridhiwani Ally Mkazi wa Ubungo jijini la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki aliibuka kuwa mshindi wa jackpot ya SportPesa kwa kujishindia kitita cha zaidi ya Sh Mil 437 na jana akakabidhiwa zawadi ya ushindi huo kwenye hafla fupi iliyofanyika ofisi za SportPesa, Masaki, Dar.

Ally mwenye umri wa miaka 35 amejishindia kitita hicho baada ya kubashiri kwa usahihi Mechi 13. Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi mfano huo wa hundi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tanzania Tarimba Abbas alimpongeza Ally kwa ushindi huo.

Tarimba alisema kuwa wao SportPesa ni kampuni isiyobahatisha katika katika michezo hiyo na ndiyo maana wamekuwa namba moja hapa nchini huku akitoa shukrani kwa Watanzania kuwafikisha hapo walipo.

“Nichukue fursa hii kumtangaza mshindi mpya wa wiki hii wa jackpot yetu ya SportPesa. Bwana Yassin, kama SportPesa tunaamini ndoto zake zitatimia baada ya kushinda jackpot hii baada ya kushinda mechi 13 kiukwei siyo kazi rahisi kwake.

“Shilingi 437,631,320 siyo ndogo kwa Mtanzania wa kawaida, lakini kama SportPesa tunafarijika tukiona maisha ya Watanzania yakibadilika baada ya kushinda na SportPesa hivyo niwatake Watanzania waendelee kubashiri nasi kwani kila wiki SportPpesa itakuwa ikitoa mamilionea.

“SportPesa tunatoa zawadi kwa kila mshindi wetu ambaye ameshinda bila kuangalia mazingira anayotokea ilimradi awe na umri kuanzia miaka kumi na nane (18).

“Tunachukua fursa hii kuwashukuru washindi wetu wa wiki hii na kuwaomba watumie vyema pesa walizojishindia kwa ajili ya kuendeleza maisha yao, pia ni faida kwa serikali ambayo kwa kupitia ushindi wake kumeinufaisha kwa kukatwa Sh Mil 87 iliyokatwa kwenye kodi.”

“Kuna washindi wengine pia waliojishindia mechi 10, 11 na 12, hivyo SportPesa tunawazawadia hata wale ambao hawakufanikiwa kubashiri mechi zote 13 kwa usahihi.”

“Lakini kikubwa kabisa ni kodi ambayo Bwana Ally atalipa kwa mujibu wa sheria za kodi sawa na asilimia 20% ya zawadi yake, kodi atakayolipa itakuwa ni Tshs. 87,526, 264 ambayo itaenda serikalini moja kwa moja, ni fahari kwetu” alisema Tarimba.

Naye Ally alisema kuwa alianza kubashiri na SportPesa kwa miezi mitano iliopita na alipata hamasa zaidi baada ya kuona washindi wa jackpot wa kitita cha Sh Mil 825 wa jackpot iliyopita.

“Nilianza kucheza na SportPesa miezi mitano iliyopita baada kuwaona Magabe na Kingslay wakikabidhiwa cheki yao, niliamini na kuanza kucheza. Nashukuru Mungu leo nimeibuka kuwa mshindi.”

“Nawashukuru sana SportPesa kwa kubadili Maisha yangu. Nimekuwa nikimiliki biashara ndogo ya kuuza vinywaji na vitafunio ili kuendesha maisha lakini nitafanya biashara kubwa ambayo angalau itakuwa na uwezo wa kunilipa vizuri, alisema.

“Leo ndio nimeamini kuwa mimi ni mshindi wa jackpot kwa wiki hii licha ya SportPesa kunipa taarifa Jumapili jioni. Nachukua fursa hii kuwaatarifu Watanzania kuwa ni ukweli kabisa SportPesa wanatoa zawadi kila mshindi anapopatikana na hivyo niwaombe wale ambao hawaamini na hawajaanza kucheza na SportPesa wafanye hivyo kwani wanaweza kupata bahati kama mimi ya kujishindia jackpot kama hii.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Michezo ya Kubahatisha Kitengo cha Ilala, Haule Philip alisema kuwa “Ushindi wa unaopatikana SportPesa unakuwa wa uwazi na ndiyo maana Yassin ambaye mshindi leo hii yupo hapa mbele kwenye vyombo vya habari.

“Ushindi huu wa Yassin umeongeza mapato serikali ambaye yeye anakatwa Sh Mil 87 ambazo zote zinaingia serikalini, kikubwa ni kumtaka mshindi huo aendelee kuzitumia pesa hizo vizuri, alisema Philip.

Naye Elibariki Sengasenga ambaye ni Mwakilishi wa Bodi wa bodi ya Michezo ya Kubahatisha kutoka serikalini alisema kuwa “SportPesa ni sehemu ya michezo ya ambayo serikali inaratibu, hivyo tuwapongeze kwa hatua waliyofikia katika michezo hii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents